Mawasiliano ndio kiini cha mahusiano yenye furaha, bila mawasiliano hakuna mahusiano. Watu wamejikuta kwenye migogoro kila siku kwenye mahusiano yao sababu ya kukosa mawasiliano mazuri
Mawasiliano yakiharibika hakuna mahusiano!.
Paul Izengo
Mtindo 1: Passive Communication (Mawasiliano ya MPITO)
Mtindo huu unaweza kuutumia kwa wewe ambaye unafanya kazi za ubize sana (utendaji mwingi), Kila mara unapokua unapata muda kidogo unahakikisha unamtafuta mtu wako kwa kumjulia hali hii itakusaidia sana kwani usifanye ubo bize sana na kazi kiasi cha kwamba ukamsahau mtu wako wa muhimu.
Utafiti unaonyesha kua ndani ya dakika 15 za kuwasiliana na mpenzi wako pasipo mwingiliano wa kitu chochote huboresha mahusiano. Kati ya kipindi kigumu kwasasa ni watu kutoa muda wao na hii ndio dhana ya kila kitu hata kwenye nyumba za ibada tunaona watu kutoa muda wao ni kitu kigumu sana yupo radhi atoe pesa lakini sio muda wake !
Ni jambo la hatari sana kwenye mahusiano yeyote kukosa muda wa mawasiliano hata kwenye swala la imani, mara ambapo utaona mawasiliano yanapungua hapohapo ndipo chanzo cha upendo kushuka ama kupoa (love fatigue) baada ya upendo kupoa yawezekana kuisha kabisa au vitu vingine na vikachukua nafasi na kumsahau umpendaye.. “Huwezi kukosa muda hata kidogo wa kuwasiliana na umpendaye wasiana naye haya kidogo muda mpito!“

Mtindo 2: AggressiveCommunication (Mawasiliano ya FUJO)
Mtu anayetumia mtindo huu mara nyingi hua ni wakulalamika, kulaumu,kususa hadi mwisho wa mawasiliano yao UGOMVI lazima utokee. Anayependa mtindo huu utaona anakutangazia maneno yake mbele kabla hujamalizia sentensi.
Kuna yule ambaye mkianza mawasiano naye anataka asikilizwe yeye tu hakupi nafasi ya wewe ya kuwasilisha hisia zako, kumbuka “Kwenye mahusiano ni vizuri mno kumsikiliza mwenzako anachoongea hata kama hakina maana kwako KULIKO kutaka wewe uweleweke!“

Mtindo 3: Passive Aggressive Communication (UKIMYA)
Kuna yule anakukalia kimya mpaka mnasahau kama mpo kwenye mahusiano, wanao tumia mawasiliano mara nyingi hua ni watu wa kusubilia atanipigia yeye, atanitext yeye, .. na kusema kama vipi apite ivi
Hawa ni wale ambao hukaa hata wiki na kila mtu anakua nalake moyoni.
Hii hali ikiendelea basi mahusiano yataenda kufa , kwani hakuna anayejali hisia kizo kiasi cha kuzitunza ila kumbuka hili kwenye mahusiano hakuna KUPIGIWA ni KUPIGIANA hakuna KUJALIWA ni KUJALIANA…
Mtindo 4: Assertive communication
Mtindo huu humpa nafasi kila mmoja kueleza hisia zake kwa mwenzake , makosa hua sio kikwazo kwao cha kuweza kuzuia mawasiliano yasifanyike . Kila mmoja humpa umakini mwenzake na kuheshimu anachosema.
Mahusiano hujengwa na vitu vigodovidogo sana mawasiliano pia huweza kuharibiwa na vitu vidogovidogo sana. Kama mwenzako amekukosea mtumie sms na kumuomba msamaha hakuna haja ya kukuaa kimya, Ukimya unamshindo mkuuu unaweza kufanya hasira ya mtu kupanda na matokeo ya hasira kupanda basi moyo wa mtu huweza kubadilika , unaweza kufikia hatua ya kughahirisha mahusiano hayo.
No matter how good DANCER you’re you must know how to leave the stage! yaani haijaishi ni namna gani unavyojua kucheza lakini unatakiwa kujua namna gani ya kuondoka jukwaani