Sonona (Depression) ni hali ya kutokua na furaha na kushindwa kuona uchanya wa jambo lolote lile linalohusiana na maisha, sambamba na kuhisi huzuni nzito na hasira.
Watu wenye njaa ya mafanikio hawatazamii ukubwa wa changamoto bali wanatazamia ukubwa wa ndoto.
Faraja Peter
Dalili za sonona (Depression) ni zipi?
i) Hali ya hasira wakati wote
ii) Kupoteza hali ya kufanya jambo
iii) Kukosa usingizi kabisa au kulala kupita kiasi
iv) Mabadiliko katika hamu ya chakula
v) Uchovu usio wa kawaida
vi) Kuhisi unyonge
vii) Kutokujiamini
viii) Ugumu katika kuzingatia mambo
Dalili hizi unaweza usiwe nazo zote ila kuna baadhi zinaweza kuwa sumbufu kwako au ndiyo inakutokea mara kwa mara
Utawezaje kudhibiti Sonona?
i) Epuka kuhufadhi mambo mengi bila kushirikisha watu/mtu unayemwamini
ii) Epuka mambo yanayochochea kusononeka ama kukaa mahali unaanza kuwa na hisia za huzuni au kulalamika juu ya jambo fulani.
iii) Fanya mazoezi mara kwa mara ili akuifanya akili yako kutokuwa inawaza jambo moja au ama kuwaza sana katika jambo linalokusumbua
iv) Zungukwa na watu wanaotambua ubora na uzuri wako
v) Jipe muda , kuwa na utulivu utafikia malengo yako!
Soma kitabu changu kinachopatikana katika kurasa ya Shop