Kabla ya yote ngono huharibu mfumo wa kufikiri! kwanini ngono imekua inaleta uharibifu sana sababu ya hatima yako!
Fikra yako ikiharibika na hatima yako inakosa mwelekeo!.
Wandowa Titus
Sababu zinzopelekea vijana kuwa na uraibu wa ngono
- Urahisi wa kupata Maudhui ya ngono (Pornography)
Teknolojia na intanet vimefanya maudhui ya ngono (porno) kuwa ni rahisi kupatikana, hivyo vijana wengi wanapata uraibu wa kutazama porno kuanzia wakiwa na umri mdogo tabia inajijenga toka wakiwa wadogo.
Ponografia huongeza tamaa zisizothibitika na mara nyingine hupelekea uhalisia wa ngono kupoteza maana yake halisi (emotional disconnection) - Ukosefu wa Elimu Sahihi ya ngono
Wengi hawapati elimu ya kina kuhusu afya ya uzazi , thamani ya miili yao na athari za kujihusisha na ngono kiholela. Matokeo yake wanajifunza kutoka kwa mitandao au marafiki ambao wengi wao hawatoi maarifa sahihi. - Shinikizo la Kijamii na Utamaduni wa kileo
Tamaduni nyingi za sasa hasa mtandaoni zinachochea kuonesha “Ngono kama burudani” badala ya kuwa tendo la heshima na dhamana. Vijana hushawishiwa kwa urahisi kupitia filamu, muziki, mitandao ya kijamii, n.k - Changamoto za Kisaikolojia
Wengine hukimbilia ngono kama njia ya kuepuka msongo wa mawazo , upweke na huzuni au matatizo ya kifamilia. Hii imepelekea tabia ya kutumia ngono kama “Dawa ya muda” kwa maumivu ya ndani(Emotional numbing) - Hofu ya kukosa (FOMO -Fear Of Misiing Out)
Vijana wengi hujihusisha na tabia za ngono kiholela kwa kuhisi wanapaswa “kuwa kama wengine” au wasibaki nyuma kimaendeleo ya kijamii (Peer Pressure) - Kutafuta Uthibitisho wa Kimaumbile
Wengine hujihusisha na ngono mara kwa mara kutafuta kuthibitisha utu wao au thamani yao (self-worth) kwa kujihisi wanapendwa au wanathaminiwa kupitia tendo la ngono.
NAWEZAJE KUSHINDA URAIBU WA NGONO?
1. KUKIRI NA KUJITAMBUA
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo inakuhitaji wewe binafsi kukiri kweli ulikosea na unataka mabadiliko
i) Kubali kweli kuna tatizo : Jitambue kuwa una uraibu wa ngono na upo tayari kilishugulikia kwa moyo wa kweli